THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

maendeleo ya mchezo wa Baseball na Softball Tanzania

Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha mchezo wa Baseball na Softball Tanzania ndugu Alpherio Nchimbi zinasema kwamba mafunzo kwa walimu pamoja na wachezaji wa Baseball Mkoani Mbeya yamekamilika kwa mfanikio makubwa ambapo zaidi ya washiriki 50 wamepata mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti vya kuhitimu. Mafunzo hayo yalitolewa na mwalimu mbobezi kutoka Japan ndugu Hiroki Iwasaki, yalianza tarehe 15 Julai na kukamilika jana Jumapili tarehe 16 Julai, 2017 yalikuwa ni ya siku nzima. "Intensive training program". Picha hizo zinaonyesha washiriki wakiwa viwanjani.
 mafunzo kwa walimu pamoja na wachezaji wa Baseball Mkoani Mbeya
 mafunzo kwa walimu pamoja na wachezaji wa Baseball Mkoani Mbeya
 Baadhi ya washiriki 50 ambao wamepata mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti vya kuhitimu wakiwa na na mwalimu mbobezi kutoka Japan ndugu Hiroki Iwasaki