Jeshi la Magereza nchini limeanza kutekeleza mpango wake wa kupanua shughuli za uzalishaji wa kiwanda cha Viatu cha Karanga  kilichopo mjini Moshi  mkoani Kilimanjaro  sambamba na kujenga Kiwanda Kipya cha Viatu  katika eneo hilo hilo ili kupanua huduma zake kwa wananchi na hivyo kukidhi mahitaji ya soko la sasa.
Hatua hii ni moja ya kati ya Mikakati ya Jeshi la Magereza nchini Tanzania linaloongozwa na Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa (Pichani juu), kuhakikisha fursa  zilizopo na wataalamu waliopo ndani ya Jeshi la Magereza nchini zinatumika na wanatumika  vizuri kwa manufaa ya watanzania wote sambamba na Jeshi hilo kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa viwanda.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dr. Juma Malewa anasema baada ya upanuzi huo ambao umeanza kufanyika mapema mwezi Juni mwaka huu kiwanda hicho kitakuwa na  uwezo wa kuzalisha  jozi 400 kwa siku na hivyo kuongeza kasi ya upatikanaji wa viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza kwa ubora kwa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ama mashine  za kisasa.
Dk. Malewa anasema awali  kiwanda  hicho kilichopo Gereza la Karanga mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kutokana na kutumia teknolojia ya zamani   kilikuwa na  uwezo wa kuzalisha jozi 150 kwa siku kiwango ambacho ni kidogo ukilinganisha na soko la sasa.
Anasema tayari Jeshi la Magereza limeingia Ubia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF   kwa lengo la kupanua  shughuli za uzalishaji  wa Kiwanda  cha Viatu cha Karanga kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro sambamba na kujenga  kiwanda  kipya cha viatu katika eneo hilo hilo. 
Dk. Malewa anasema  katika kutekeleza azma yake ya ujenzi wa Kiwanda kipya  cha Viatu tayari zimetengwa ekari 20 kwa ajili ya kiwanda hicho katika eneo hilo la Karanga mjini Moshi na kwamba eneo hilo hilo litakalotumika kujenga Kiwanda  cha Viatu pia litatumika kujenga Kiwanda cha Soli na Kiwanda cha kuchakata Ngozi na kwamba Kiwanda hicho kinategemewa kukamilika mapema Julai mwaka 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...