Rais wa Shirikisho Ngumi za Kulipwa TPBC,  Chaurembo Palasa.



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.



KESI iliyokuwa imefunguliwa katika Mahakama kuu na Kampuni Tatu za kuendesha biashara ya Ngumi Tanzania imetupiliwa mbali baada ya kushindwa kukidhi Vigezo.

Kampuni hizo za Puglist Syndicate of Tanzania (PST), Tanzania Professional (TPBO) na Tanzania Proffesional boxing Limmited zilifunguwa kesi ya kupinga kusajiliwa kwa Tanzania Proffesiona Boxing Commision na Baraza la michezo la Taifa.

Katika Kesi hiyo Kampuni hizi ziliungana ili kutaka "BMT" ieleze kwanini walikipa usajili chama cha kusimamia Ngumi za kulipwa wakati hawana uwezo wa kusajili michezo ya kulipwa.

Akizungumza kwa Simu kutoka Dar es salaam Rais wa Shirikisho lililoshtakiwa Chaurembo Palasa alisema Kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na Jaji Kihiyo imetupwa baada ya kutokidhi vigezo kisheria.

Alisema kesi hiyo ilifunguliwa na Emanuel Mrundwa Katika Mahakama  ya Temeke lakini ilishindwa kusikiliza shauri hilo kutokana na kukosa nguvu kisheria. Kesi hiyo ilielekezwa na kupelekwa Mahakama kuu ndipo Kampuni zilipoungana na kuomba kusikilizwa huku wakiishtakiwa wakiongezeka kuwa TPBC na BMT.

BMT na TPBC ililazimika kutoa vielelezo vya kupinga kushtakiwa na Kampuni hizo kutokana na Baraza hilo kuwepo kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Kutokana na ombi lao kukosa vigezo vya Kisheria Mahakama Kuu imeamuwa kuliondowa Shauli hilo na kuwataka walalamikaji kulipa Gharama za kesi. Gharama za kesi hazikuweza kujulikana mara moja kutokana kuandaliwa ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali. Kutokana na kushindwa kwa kesi hiyo TPBC itabaki kuwa Kamisheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania na sasa inapaswa kuendelea na mchakato wa kuwa na vyama vya Mikoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...