Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu imekwama kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili video Queen, Agnes Gerald 'Masogange' kwa sababu ana tatizo la kiafya.
Hayo yameelezwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Wilbard Mashauri baada ya wakili wa serikali, Costantine Kakula kueleza shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.
Hata hivyo, wakili wa Masogane, Ruben Simwanza alimueleza Hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi iahirishwe.
Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 25, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...