Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imelazimika kuhamishia shughuli zake katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa muda kumsomea mfanyabiashara Yusufali Manji (41), mashitaka ya uhujumu uchumi yanayomkabili.

Manji amesomewa mashtaka hayo katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitalini hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Huduma Shaidi.

Katika kesi hiyo, Manji anashitakiwa pamoja na wenzake watatu, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43)  mkazi wa Chanika, ambapo wote watatu wamesomewa mashtaka yao katika Mahakama hiyo kabla haijahamia hospitali ya Muhimbili kuanzia muda wa saa Tisa alasiri na kumalizika saa 16:41 (saa kumi na dakika arobaini na moja).

Mahakama ilifikia uamuzi wa kuhamia Muhimbili baada ya Manji kuwa amelazwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na kulazimika kusomewa mashtaka yake akiwa kitandani.

Akisoma mashtaka hayo, wakili Mwandamizi wa Serikali, Tulumanywa Majigo amedai kwamba Juni 30, mwaka huu huko Chang’ombe A wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja, walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea  sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vyenye thamani ya milioni 192.5.
Imedaiwa kuwa, Julai Mosi mwaka huu, maeneo hayo hayo, washitakiwa  wote walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo nane ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za JWTZ vyenye thamani ya milioni 44.

Aidha imedaiwa kuwa, Juni 30, washitakiwa hao walikutwa wakiwa na mhuri wa JWTZ ambao uliandikwa ‘’Mkuu wa Kikosi 121  Kikosi cha JWTZ’’ bila kuwa na uhalali,  kitendo kinachohatarisha usalama wa nchi.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...