Mbunge wa Ilala ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge Mhe Mussa Azzan Zungu  akiongoza kikao baina ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda  na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kikao baina ya Makamishina hao ambacho lengo kubwa lilikuwa ni kubadilishana uzoefu wa utedaji kazi kiliongozwa na Mhe Zungu  kwa niaba ya Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania. Makamishina hao wa Bunge la Uganda wapo nchini kwa ziara ya Kibunge ya siku mbili.
 Kiongozi wa Msafara Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda Mhe Cecilia  Ogwal (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa kikao baina ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda  na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Bunge mbaye pia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania Dkt. Thomas Kashililah akizungumza wakati wa  kikao baina ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda  na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda  na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania  (waliokaa) na baadhi ya Watumishi wa pande zote mbili katika  picha ya pamoja mara baada ya kikao.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...