THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Makamu wa Rais apongeza juhudi za MERCK nchini Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  amezipongeza juhudi zinazofanywa na taasisi ya Merck ambayo ni kampuni inayoongoza katika sayansi na teknolojia  ambayo imelenga  kushughulikia masuala  uwezeshwaji wa wanawake na huduma za afya akisema kwamba wamekuja nchini  kwa wakati mwafaka, 
Wakati wa mkutano maalum kati ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck Foundation  Makamu wa Rais  alisema kuwa Merck Foundation  inakaribishwa na serikali inatarajia kushirikiana  na taasisi hiyo  inayoheshimika na iliyo makani katika  kuwezesha wanwake , vijana, huduma za afya  na sayansi. 
Tunatambua mchango  unaotolewa na Merck Foundation  katika kujengea uwezo  huduma za afya barani Afrika na tunakaribisha shughuli zake  nchini Tanzania, hususani katika kampeni zinazolenga  kuuongezea umma  uelewa kuhusu ugumba. 
Makamu wa Rais aliongeza, “Mimi binafsi nitafanya kazi na Merck katika kuwawezesha wanawake walio na uwezo duni kijamii na kiuchumi kote nchini Tanzania  na sehemu nyingine duniani ili kujenga utamaduni mpya  katika kuheshimu na kumtambua wanawake  kama sehemu ya wanajamii wanaozalisha  wawe ni kinamama na hata wasio wazazi.” 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha Ofisa Mkuu Mtendaji wa Merck Foundation, Dk Rasha Kelej,  ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ofisa Mkuu Mtendaji wa Merck Foundation, Dk Rasha Kelej,  ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam.