THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAKAMU WA RAIS AREJEA NCHINI AKITOKEA NCHINI ETHIOPIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amerejea nchini akitokea jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU). Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Makamu wa Rais wa akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaviva . Katika Ujumbe wa Mkutano huo Makamu wa Rais pia aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.