WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, viongozi waandamizi wa Serikali na mamia ya wananchi kuuaga mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Bw. Hassan Shebuge. 
Marehemu Bw. Shebuge ameagwa leo (Ijumaa, Julai 7,2017) nyumbani kwake Mbagala- Majimatitu jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi, Julai 8, 2017), katika kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga. 
Bw. Shebuge amefariki dunia jana (Alhamisi, Julai 6, 2017) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata na shinikizo la damu. 
Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali. 
Amesema enzi za uhai wake marehemu Bw. Shebuge alikuwa mpole na muadilifu na kutoa  mchango mkubwa kwenye kufanikisha maamuzi na utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa ufanisi. 

“Kwa kweli hatuna budi kwa sasa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.” 
Awali, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata akisoma wasifu wa marehemu Bw. Shebuge alisema marehemu alizaliwa Mei 25, 1969 wilayani Korogwe, Tanga.

Alisema marehemu alipata elimu ya msingi katika shule ya Mkwakwani kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1983, ambapo alipata elimu ya sekondari katika shule ya Usagara kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987, zote za mkoani Tanga. 
Bw. Kidata alisema mwaka 1988, marehemu alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mkoani Arusha kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na cha sita.  
Alisema mwaka 1992 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada ya Sanaa na Ustawi wa Jamii mwaka 1995, mwaka 1998 alipata shahada ya uzamili ya Sanaa na Ustawi wa jamii. Pia marehemu alipata mafunzo mengine mbalimbali ndani na nje ya nchi.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu, Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akishiriki katika Dua ya kumuombea Marehemu Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
 Sehemu ya Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge pindi ulipowasili nyumbani kwake, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo tayari kwa maandalizi ya mazishi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...