Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea gereji inayotengeneza  Magari ya RSA Limited  ya mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kukagua maendeleo ya ukarabati na ubadilishaji mwonekano wa Magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi yaliyosafirishwa kwenda huko hivi karibuni.
Akiwa katika gereji  hiyo Mhe. Makonda amejionea magari hayo yakiwa katika hatua mbalimbali za utengenezaji ambapo ameomba uongozi wa kampuni hiyo kukamilisha ukarabati wa magari hayo kwa wakati iliyaweze kuongezea ulinzi na usalama jijini Dar es salaam.
Aidha RC Makonda amesema kuwa anataka kubadili mwonekano wa jeshi la polisi Mkoa wa Dar es salaam kwa kuhakikisha magari ya polisi yanakuwa na hali nzuri itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa uufanisi kwa kuyabadili magari hayo kuwa kama yale ya Askari wa umoja wa mataifa.

”Hakuna kitu kinachoninyima usingizi kama pale mwananchi anapohitaji polisi wafike mahala pa tukio na polisi hawafiki, na kufanya hali ya amani kutoweka na wakati huohuo polisi wanataka kufanya kazi yao ila wanashindwa kutokana na uhaba wa vifaa.
"Hii ndiyo sababu ninahangaika ili siku moja Dar es Salam iwe na amani hata kufikia hatua ya watu kufanya biashara zao kwa masaa 24 na kutembea kwa amani muda wote", alisema  RC Makonda.
"Nimepata Pikipiki 200, baiskeli 500 na  kutengeneza magari haya 56 kuwa na viwango vya kimataifa kama magari ya Umoja wa Mataifa yanavyoonekana
"Yaani kwenye gari ya doria itaweza kuwa na maafisa wa polisi tisa kwa nyuma, ambao watatu watakuwa kushoto na watatu kulia mwa gari hiyo huku wawili wakiwa nyuma ya gari hiyo na mmoja akiwa amesimama mbele na silaha kubwa", aliongeza  RC Makonda.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26 ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika gereji  ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro kwa ukarabati ili yaendane na kazi ya jeshi la p0lisi
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akijadiliana jamabo na uongozi wa gereji  ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro wakati alipokagua magari ya polisi yanayofanyiwa ukarabati mkubwa.
Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akiakizungumza na uongozi wa gereji  ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa mkoa wa Dear es salaam Mhe. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26 ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...