MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema miongoni mwa Makampuni Binafsi yanayoisaidia Serikali kwa kufanya kazi ya uuzaji na upimaji wa Viwanja vya Viwanda na Makazi, ni Kampuni ya Property International pekee ambayo mpaka sasa kama mkuu wa mkoa bado hajapata malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu migogolo ya ardhi.

Akizungumza katika Kipindi cha Sema Kweli kinachorushwa kila Ijumaa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, alisema kuwa, amekuwa akipata malalamiko kadhaa kutoka kwa wananchi juu ya migogolo hiyo inayotokana na kuuziwa ama kupimiwa viwanja na makampuni ambayo hayajajitosheleza katika kufanya kazi hiyo baada ya kuidhinishwa na Serikali.

Aidha alisema kuwa kutokana na suala hilo kumekuwa na ugumu wa Serikali kukusanya mapato 'Kodi ya majengo' kutokana na wananchi kujijengea makazi holela bila kupata vibali vya ujenzi, baada ya kuuziana maeneo kienyeji bila kupimwa na kupatiwa hati, jambo ambalo kwa sasa linafanyiwa kazi kwa kasi na baadhi ya makampuni binafsi ikiwamo ya Property International, yanayoshirikiana na Selikali katika kifanya kazi hiyo.

Makonda alimpongeza Waziri William Lukuvi, kwa kazi ngumu anayofanya ikiwa ni pamoja na ya ulasimishaji wa makazi ili kwenda na viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya kuzitambua nyumba na kuzipa madaraja tofauti kurahisisha upatikanaji wa kodi ya majengo, na mpangilio wa miji unaotakiwa huku Serikali ikiendelea kuwakaribisha wapimaji biasfi ili kuendana na kasi.

''Wapimaji binafsi watasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa Watumishi na Vifaa vya kisasa vinavyorahisisha upimaji wa haraka na kwa wakati, lakini Manispaa zinatakiwa kuwapa ushirikiano makampuni hayo kwa kuwapa na kuwatambua ili Serikali inapotoa Hati isitokee mgongano kutokana na maeneo husika kupimwa na watu watatu tofauti''. alisema.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...