THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAMA JANETH MAGUFULI ATOA MISAADA MBALIMBALI KWA WAZEE WASIOJIWEZA 400 CHATO MKOANI GEITA





Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo Ijumaa  Julai 07, 2017 amekutana na wazee wasiojiweza wa Wilaya ya Chato na kutoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa lengo la kuwapunguzia changamoto zinazowakabili. 
Mama Janeth Magufuli amekabidhi msaada huo kwa wazee zaidi ya 400 kutoka kata 23 za Wilaya ya Chato mkoani Geita
Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo kwa wazee hao wa Chato Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ameitaka jamii,watu binafsi,wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali kushirikiana kwa pamoja katika kuwasaidia wazee hapa nchini. 
Mama Janeth amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wazee hao kuwa ni pamoja na vyakula,madawa na hata upendo na kuthaminiwa. 
“Tunawaomba jamani mnaokaa na wazee muoneshe upendo,muwasaidie pale wanapohitaji msaada,kama wewe una nguvu basi msaidie hata kuchota maji na kukata kuni kwani hizo ndo Baraka zenyewe” 
Kwa upande wao wazee hao wamemshukuru mke huyo wa Rais kwa moyo wake wa kujitolea hususani katika kuwasaidia wazee na wasiojiweza huku wakiiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza changamoto zinazowakabili wazee. 
Awali akisoma risala kwa niaba ya wazee hao mbele ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Afisa Maendeleo wa Jamii Lidiana Kasheku amemueleza Mama Janeth namna Halmashauri hiyo ilivyojipanga kutatua kero za wazee hao ikiwa ni pamoja na kuanzisha Baraza la Wazee litakalosaidia kubaini changamoto na aina ya msaada wanaouhitaji sambamba na kutoa kipaumbele kwa wazee katika huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na suala la matibabu kwa wazee.
Mama Janeth Magufuli amekabidhi vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mchele, Unga wa Mahindi,Mafuta ya Kula, Sabuni za kufulia na Maharage. 
Wilaya ya Chato mkoani Geita ina vijini 115 vyenye wazee zaidi ya 18,000 ikiwa ni sawa na asilimia 5 ya wazee wote nchini barani Afrika.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwakabidhi kwa pamoja mafuta waakilishi wa Wazee kutoka kata ya Kasenga AnatoryBisate (64) kulia pamoja na Bi. Winfrida Lawrent(65) kushoto mara baada ya kuzungumza na wazee 400 katika Ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiimba pamoja na wanakwaya wa Mwagazege mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Wazee wasiojiweza zaidi ya 400 kutoka Wilaya ya Chato katika Ukumbi wa Mshikamano Saccos.