THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAMLAKA YA UDHIBITI WA MANUNUZI YADHAMIRIA KATIKA KUBORESHA MANUNUZI YA BIDHAA NA VIFAA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MAMLAKA  wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)imejizatiti kwa kufanya marekebisho ya sheria ikiwa ni katika kuboresha zaidi manunuzi ya bidhaa na vifaa kwa serikali.

Akizungumza wakati akitembelea banda la PPRA lililopo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt Laurent Shirima amesema kuwa maboresho hayo yatalenga katika sehemu tano ambazo zitaboresha manunuzi ya zabuni katika nyanja mbalimbali.

Dkt Shirima amesema kuwa sheria hiyo imeboreshwa katika kupunguza gharama za ununuaji wa Bidhaa na vifaa, serikali kununua kwa bei za sokoni wakimaanisha bei halisi ya bidhaa na vifaa pia wametoa upendeleo kwa makampuni ya ndani ikiwemo makundi maalumu kama vile wanawake, wazee na vijana.

Ameongezea kuwa, katika maboresho mengine yaliyofanywa ni katika kuendeleza viwanda kama serikali ya awamu ya tano inavyosisitiza ukuaji wa viwanda huku PPRA ikiangalia zaidi wataalamu wa manunuzi kutoka ndani pia wapo katika hatua za mwisho za kuhamia katika mfumo wa kieletroniki wa ununuzi wa zabuni.

PPRA ni mamlaka inayohusiana na udhibiti wa manunuzi ya Umma ambapo kupitia kwa Mtendaji Mkuu Dkt Shirima amewaondoa hofu wananchi kuwa waiamini taasisi yao kwani mambo mengi ya msingi yameshawekwa wazi na fedha za umma zinahitaji uwajibikaji.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma  PPRA Dkt Laurent Shirima akizungumza na wanahabari wakati alipotembelea banda la Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma PPRA lililopo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango na kuelezea namna wanavyojizatiti katika kuboresha ununuaji wa zabuni kwa serikali.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt Laurent Shirima akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda lao na katika maadhimisho ya 41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt Laurent Shirima akipata maelezo kutoka kwa  mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa Taifa (PPF) wakati alipotembelea banda hilo lilipo katika Jengo la Wizara ya Fedha na Mipango  katika maadhimisho ya  41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.