NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaahidi wananchi wanaojitokeza kwenye banda la Mfuko huo, lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, kuwa wataendelea kupatiwa huduma zote kama ambazo wamezoea kuzipata kwenye ofisi za Mfuko huo kote nchini.

Ahadi hiyo imetolewa leo Julai 6, 2017 na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi waliofika kupatiwa huduma mbalimbali zikiwemo zile za wanachama kujua michango yao, wananchi kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), ambapo mtu aliyejiunga na mpango huo husajiliwa na kupatiwa kitambulisho papo kwa hapo.

"Leo idadi ya watu imeongezeka sana bila shaka wamevutiwa na huduma zetu na tunawahakikishia tutaendelea kutoa huduma bora na za haraka hadi tarehe ambayo maonesho haya yatafikia kilele kama alivyoagiza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa siku za maonesho zimeongezeka hadi Julai 13, 2017 badala ya Julai 8." Alifafanua Bw. Njaidi.

Idadi kubwa ya wananchi waliofika kwenye banda hilo ni wale wajasiriamali ambao wengi wamejiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari ambapo moja ya faida kubwa ya kujiunga na mpango huo ni kupata fao la bima ya afya inayomuwezesha mwanachama kupatiwa matibabu yeye na wategemezi wake kwenye hospitali zilizoaishwa kote nchini.

Win-God Simon, (kushoto), Afisa wa PSPF akiwahudumia wananchi na wanachama wa Mfuko huo waliotembelea banda la PSPF leo Julai 6, 2017

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw.Erick Shitindi(kulia), akipokea vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko wa Pensehni wa PSPF kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi wakati alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 6, 2017.

Wananchi waliofurika wkenye banda la PSPF, leo Julai 6, 2017
Bw. Costa wa PSPF, (kushoto), akifafanua jambo kwa wananchi hawa waliofika kwenye banda la PSPF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...