THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAONESHO YA SABASABA 2017; WAAJIRI NA WAFANYAKAZI WAJITOKEZA KWA WINGI BANDA LA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) KUPATA ELIMU ZAIDI KUHUSU MFUKO HUO


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAAJIRI na wafanyakazi wamejitokeza kwa wingi kupata elimu kuhusu kazi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.

Maonesho hayo ya kila mwaka huwaleta pamoja wafanyabiashara ya makampuni makubwa ya kimataifa kutoka nje na dnani ya nchi, lakini pia kunakuwepo na mkusanyiko mkubwa wa wafanyakazi wa umma na binafsi wanaotoa huduma mbalimbali kwa watu wanofika kutembeela maonesho hayo.

Mfuko wa Fidia kwa wWafanyakazi, (WCF) imetumia fursa hiyo kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi ambao walifika kwenye banda la Mfuko huo na kupatiwa maelezo ya kina kuhusu kazi za Mfuko kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wake Bw. Masha Mshomba, wakurugenzi na wakuu wa idara pia.

“WCF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ulioanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 5 ya Fidia kwa Wafanyakazi kifungu namba 263 ya mwaka 2015.” Bw. Mshomba aliyasema hayo akiwa kwenye banda hilo ambapo waajiri na wafanyakazi walifika kupata elimu zaidi ya kuhusu Mfuko huo.

Bw. Mshomba aliendelea kufafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria iliyoanzasha Mfuko huo, tofauti na Mifuko mingine ya Hifadhio ya Jamii, ambapo mwajiri na mfanyakazi hutoa michango ya kila mwezi, kwa upande wa WCF, ni mwajiri pekee ndiye anawajipika kumchangia mfanyakazi wake kila mwezi na mfanyakazi hawajibiki kutoa mchango wowote.

 Aidha Bw. Mshomba alieleza kuwa, dhumuni kuu la kuanzishwa kwa Mfuko huo ni kutoa Mafao ya kutosha na stahili  kwa Mfanyakazi aliyepatwa na maradhi au majeraha yaliyotokana na kazi anazozifanya Mfanyakazi huyo.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar, akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akizungumza wakati akiwa kwenye banda la Mfuko huo.

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akizungumza na Posta Masta Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Deo Kwiyukwa, wakati alipotembelea banda hilo.
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar, akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF.
 Wafanyakazi hawa wakipatiwa maelezo mbalimbali yahusuyo huduma zitolewazo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA