Na Francis Godwin, Iringa
SERIKALI ya wilaya ya Kilolo na mbunge wa kilolo Mhe. Venance Mwamoto wamewapongeza kwa zawadi za maandalizi ya chuo kikuu mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (19) waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu. 
Wakikabidhi zawadi hizo kwa mapacha hao jana mbele ya walezi wao wa kituo cha Nyota ya asubuhi ambako wanaishi Maria na Consolata, Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah, Mhe.Mwamoto ambao waliongozana na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kilolo Bw. Alloyce Kwezi na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo Seth Moto walisema wamevutiwa na ufaulu wa mapata ambao ni yatima hivyo wamelazimika kuwaanzishia maandalizi ya chuo mapema zaidi kwa lengo la kuwawezesha kuanza chuo kwa wakati.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo Kwezi alisema kwa kufanya kwao vizuri kumeongeza heshima kubwa kwa wilaya ya Kilolo ambayo ndio iliyoongoza kwa matokeo ya kidato cha sita kwa mkoa wa Iringa wenye shule 25 huku wilaya hiyo ikiongoza kimkoa kwa kuwa na shule Pomerini ndio iliibuka ya kwanza kwa shule zote 25. 
Hivyo alisema moja kati ya mkakati wa Halmashauri ya Kilolo ni kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mitihani mbali mbali pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo ili kuifanya wilaya hiyo kuwa mbele kwa kila jambo . 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo alisema kuwa pamoja na wilaya kutoa msaada huo kwa watoto hao mapacha kama sehemu yao ya maandalizi ya chuo bado milango ipo wazi kwa wadau wengine walioguswa na watoto hao kuzidi kuwasaidia kwani wao wenyewe wameonyesha nia ya kuendelea na masomo na kuwa mfano kwa baadhi ya jamii ambayo imekuwa ikiwaficha watoto wenye ulemavu kwenda shule .
 “ Wametuowezesha wilaya yetu kufanya vizuri kweli! Tunawapongeza wao ,walimu na wadau wote wa elimu zaidi wanafunzi ambao wamefanya vizuri katika mitihani hiyo.
"Kilolo ilikuwa ikitazamwa sana kuona nini matokeo ya  Maria na Consolata ila bila viongozi na wadau wengine wa elimu kujitoa kwa ajili yao yawezekana wasingefanya vizuri …..tupo pamoja nao na tutaendelea kuwa pamoja zaidi hadi chuo “ Mkuu huyo wa wilaya alisema.
Aliongezea kuwa moja kati ya mahitaji yao makubwa kwa sasa ni nyumba yao maalum kwa ajili ya kuishi pindi watakapokuwa chuo kwani wao wanahitaji nyumba maalum ambayo ni rafiki zaidi na aina ya ulemavu waliokuwa nao . 
Mbunge wa Kilolo Mwamoto mbali ya kuwapongeza mapacha hao bado alitaka wananchi wote wenye watoto wenye ulemavu kuiga mfano wa mapacha hao na hatapendezwa kuona watoto wenye ulemavu wa aina yeyote ile wanafichwa majumbani . 
Pia alisema moja kati ya mkakati wake kuona mazingira ya shule mbali mbali katika wilaya ya Kilolo yanakuwa rafiki na kuwataka wananchi kuendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa ,maabara ili kuepukana na changamoto ya miundo mbinu ya elimu pamoja na kwenda sawa na serikali ya Rais Dkt John Magufuli ya uboreshaji wa elimu .
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah, mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo Seth Moto wakiongea na watoto hao
mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto akiwapongeza mapacha walioungana mapacha Maria na Consolata Mwakikuti 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah akiwapongeza mapacha walioungana mapacha Maria na Consolata Mwakikuti 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah akiwapa zawadi ya laptop  mapacha walioungana mapacha Maria na Consolata Mwakikuti 
 Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti wakipokea mito
 Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti wakipokea mablanketi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...