Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kulia) akionyeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Afande Francis Massawe (kulia), jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoani humo ambalo limekwama ujenzi wake  mjini Babati mkoani humo. Mhe Masauni amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa kutembelea ofisi mbalimbali zilizopo ndani ya Wizara yake.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Afisa Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Juliette Sagamiko (kushoto) alipokua anatoa maelezo kuhusu Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji mkoani humo (linaloonekana nyuma ya viongozi hao), ambalo lipo katika hatua ya mwisho kukamilika lakini limekwama kuendelea na ujenzi wake. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Afande Francis Massawe. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akipokea salamu ya heshima kutoka kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara. Watatu kulia ni Kamanda wa Jeshi hilo, mkoani humo, Heriel Kimaro. Masauni amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa kutembelea ofisi mbalimbali zilizopo ndani ya Wizara yake. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Afande Francis Massawe, wakati alipokua akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Jeshi hilo ofisini kwake mkoani humo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...