Na Felix Mwagara (MOHA).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Manyara
kufungua Kituo cha Polisi katika Makazi ya Kabila la Wahazabe wanaoishi
katika Bonde la Yueda Chini, wilayani Mbulu.
Masauni alisema hayo jana wakati
akizungumza na mamia ya wananchi wa kabila hilo mara baada ya kukagua
jengo la mifugo katika eneo la bonde hilo ambalo jamii hiyo ilijitenga
kwa kuweka makazi pembezoni mwa Mji wa Mbulu.
“Hivi karibuni Kituo cha Polisi
kitafunguliwa hapa ili kulinda usalama wenu katika eneo hili ambalo
lilikua halina kituo cha Polisi kwa miaka mingi. Serikali ya Rais
Magufuli ni sikivu ndio mana nimekuja hapa kuwasikiliza matatizo yenu na
kuwatekelezea.” Alisema Masauni huku akishangiliwa na wananchi hao.
Aliongeza kuwa, mchakato wa
kujenga kituo hicho umeanza na tayari ametoa maelekezo kwa Kamanda wa
Jeshi la Polisi wa Mkoa huo, kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mbulu, Wabunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini na Mbulu Mjini.
Pia aliongeza kuwa, uhalifu
katika eneo hilo sasa umepata tiba kwa maana Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na wananchi watahakikisha hali ya usalama unaimarishwa
zaidi katika eneo hilo ambalo lipo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay (wapili kulia) wakicheza ngoma ya Wabarbaig/Watatoga kabla ya Masauni kuzungumza na mamia ya wananchi wa Kabila maarufu la Wahazabe na makabila mengine yaliyopo katika Bonde la Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi mkoani humo, kujenga Kituo cha Polisi kwa uharaka ili jamii hiyo ambayo inaishi pembezoni mwa mji wa Mbulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi wa Kabila maarufu la Wahazabe na makabila mengine yaliyopo katika Bonde la Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi mkoani humo, kujenga Kituo cha Polisi kwa uharaka ili jamii hiyo iweze kupata ulinzi wa kutosha katika eneo hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akijadiliana na maafisa wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara pamoja na watendaji mbalimbali wa wilaya hiyo, ndani ya jengo la mifugo lililopo Yaeda Chini katika makazi ya Wahazabe, ambalo linatarajiwa kufunguliwa Kituo cha Polisi. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara (RPC), Francis Massawe, na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwafafanulia jambo Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini, Zakaria Isaay mara baada ya Naibu waziri huyo kukagua Jengo la Mifugo (nyuma yao) ambalo linatarajiwa kufunguliwa Kituo cha Polisi ili kuwasaidia wananchi wa kabila la Wahazabe na wengineo wanaoishi katika Bonde la Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kuleta ulinzi wa raia hao pamoja na mali zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...