THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MASAUNI AWATAKA MAAFISA UHAMIAJI, POLISI KUONGEZA KASI KUCHUNGUZA NA KUWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU TANGANaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Viongozi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara yake, mkoani Tanga wakati kiongozi huyo alipofanya ziara yake kikazi mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni aliwahasa viongozi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma zaidi na kuwahakikishia kero zote walizompa atahakikisha anazifanyia kazi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakulyamba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto) akimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) alipokua anatoa taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni aliwataka Maafisa Uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakuliamba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akitoka kulikagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga ambalo linahitaji matengenezo ili kulirudisha katika hali yake ya kawaida. Hata hivyo, Masauni alimuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba (kulia) kuhakikisha jengo hilo linatengenezwa haraka iwezekavyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimfafanulia jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Zena Saidi, kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao ambayo yalifanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Masauni aliwataka maafisa uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.