THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE.Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde ameendelea kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo leo amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero ya maji katika kijiji cha Matumbulu.

Mavunde amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero hiyo kwa kutoa mabomba ya kusambazia maji kijiji kizima yenye urefu wa Kilomita 1 yenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 8.

Kufuatia utekelezaji huo wa ahadi hiyo, wananchi hao walishikwa na butwaa kwa uharaka wa utekelezaji wa ahadi hiyo kwakuwa tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika eneo ilikuwa ya muda mrefu hali iliyosababisha wananchi kutumia maji yasiyo safi na salama.

Wananchi walikuwa wanakosa fursa ya kupata maji kwa urahisi na hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na muda mwingine kutumia maji ambayo si safi na salama kutoka na umbali wa kufuata maji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Matumbulu Alfred Malogo, amefurahishwa na utekelezaji wa ahadi hiyo na kwamba alichokifanya Mavunde kuwapatia wakazi wa kijiji hicho mabomba kwa ajili ya kusambazia maji kitatatua kero yao ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu kwa wananchi.

.Mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na Diwani wa Kata ya Matumbulu Emmanuel Chibago.