Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mke wake wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika mapema loe mchana nyumbani kwao katika Kijiji cha Ikolo, wilayani Kyela mkoani Mbeya. Waziri Mkuu ameongoza mamia ya watu katika mazishi hayo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mke wake kwenye mazishi yake yaliyofanyika mapema loe mchana nyumbani kwao, katika Kijiji cha Ikolo, wilayani Kyela mkoani Mbeya. 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika mapema loe mchana nyumbani kwao katika Kijiji cha Ikolo, wilayani Kyela mkoani Mbeya
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe aliyekuwa Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, ukiwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Ikolo, wilayani Kyela mkoani Mbeya. mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe unatarajiwa kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya Milele mchana huu katika Makaburi ya familia, Kijijini kwao Ikolo, wilayani humo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akilakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel alipowasili nyumbani kwa Dkt. Harrison Mwakyembe, Kijijini Ikolo, wilayani Kyela, tayari kwa Mazishi ya Marehemu Linah George Mwakyembe aliyekuwa Mke wa Dkt. Mwakyembe.
Prof. Mark Mwandosya akimfariji Dkt. Harrison Mwakyembe aliyefiwa na Mkewe, Linah George Mwakyembe wakati maandalizi ya mazishi yake, Kijijini kwao Ikolo, wilayani Kyela mkoani Mbeya.  Kushoto ni Mke wa Prof. Mwandosya, Bi. Lucy Mwandosya.
Wakuu wa Mikoa ya Lindi na Njombe, Godfrey Zambi (kushoto) na Ole Sendeka (kulia) wakiwasili nyumbani kwa  Dkt. Harrison Mwakyembe, Kijijini Ikolo, wilayani Kyela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...