THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Mbunge wa Morogoro Mjini akabidhi milioni 20 za Biko kwa mshindi wao

MBUNGE wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, leo mjini hapa, amemkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko, Elizabeth Damian, aliyetangazwa mshindi katika droo ya 22 ya bahati nasibu hiyo inayojulikana pia kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyofanyika juzi Jumatano, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 mjini Morogoro jana, Mbunge Abdulaziz, alisema bahati nasibu ni mchezo unaoweza kutoa fursa nzuri kiuchumi, huku akimtaka mshindi huyo azitumie vizuri pesa zake ili ziweze kumnufaisha kiuchumi.

Alisema kwamba jinsi mchezo wa Biko unavyochezeshwa ni sehemu muafaka ya kuhakikisha kwamba kila mtu anatumia vyema fursa ya kupiga hatua kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, hivyo wananchi wake wa Morogoro na Watanzania wote kwa ujumla waendelee kucheza ili wavune fedha za ushindi.

“Wakati nawapongeza Biko kwa kubuni michezo hii inayotoa mamilioni kwenu washindi, lakini pia nakupongeza wewe mwananchi wangu wa Morogoro kwa kuwa kati ya wachezaji wenye bahati kubwa kiasi cha leo kukabidhiwa Sh Milioni 20,” Alisema.

Akizungumzia ushindi wake, Elizabeth aliyekabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, mjini Morogoro, alisema hakuamini kama angeweza kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka Biko, jambo linalomfanya furaha yake isielezeke.

“Kwa kweli siamini kama leo nimekabidhiwa fedha zangu kiasi cha Sh Milioni 20 nilizopata kutoka kwa Biko, hivyo nawakumbusha Watanzania wenzangu kucheza kwa wingi bahati nasibu hii maana ushindi upo nje nje na fedha zangu nitazitumia vizuri kwa mambo mengi kama vile biashara na ujenzi wa nyumba,” Alisema.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, kushoto akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 mshindi wa Biko Morogoro saa chache kabla ya kukabidhiwa fedha taslimu katika benki ya NMB, mjini hapa jana. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood wa tatu kutoka kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku, mshindi wa Morogoro Mjini, Elizabeth Damian wa pili kutoka kushoto. Wa kwanza kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wakati wanamkabidhi mshindi huyo katika Tawi la benki ya NMB Morogoro jana.
Mshindi wa Shilingi Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Elizabeth Damian baada ya kukabidhiwa jana mjini Morogoro.