Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WAZIRI wa afya, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi, Dk. Mpola Tamambele, kutokana na kushindwa kusimamia maelekezo ya serikali ya kuhakikisha mama mjamzito, mtoto chini ya miaka mitano na mzee wanapata huduma bure.
Kutokana na kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Beda Mmbaga kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo mara moja wakati uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zikiendelea.
Amemuelekeza Kaimu Mkurugenzi huyo pia kuwafuatilia watumishi wa afya kituoni hapo waliohusika kumuagiza mama aliyejifungua Salma Khalifan kwenda kununua vifaa vya kujifungulia vya sh.180,000 ili apate huduma.
Aliyasema hayo wakati alipokwenda kutembelea kituo cha afya Mlandizi, kabla ya kukabidhiwa kwa magari ya wagonjwa matatu kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo, Mhe. Hamoud Jumaa.
Mhe. Mwalimu alisema hatokubali kuona watumishi wachache kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali wanachezea maagizo ya serikali. Alifikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mama aliyejifungua ambae alisema amenunua vifaa vya kufanyiwa operesheni kwa gharama ya sh .180, 000.Ummy alisema haiwezekani kuona mama wajawazito, wanalipishwa hadi gloves na pamba ili kujifungua wakati serikali yao ilishasema watahudumiwa bure . Alieleza kwamba, kuanzia sasa waganga wakuu wa wilaya, mikoa na watumishi wa afya wote nchini wahakikishe wanatimiza maelekezo ya serikali kuhudumia akinamama wajawazito na watoto ili kupunguza vifo vya uzazi . 
Mhe. Ummy alisema kuwa ,watumishi na wauguzi wengi wanajituma na kufanya kazi zao kifanisi ila wapo wachache ambao wanakwamisha juhudi hizo.
"Sitokubali mtumishi anakwenda kinyume na serikali ,rais wetu John Magufuli anasisimamia suala zima la kuboresha huduma za afya ,halafu akitokea mtu mmoja mzembe anatuchanganya kwakweli sitoweza kumfumbia macho.
"Wananchi wamekuwa waoga hata kuingia katika suala la bima ya afya kwa sababu ya mambo kama haya ,namsimamisha mganga mfawidhi huyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika ." alisema Mhe Waziri.
Mbali ya hayo Waziri  huyo alibainisha kuwa bajeti ya dawa katika halmashauri ya  wilaya ya Kibaha imeongezeka ndani ya miaka miwili mfululizo kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya tano .


Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipata maelezo tembelea kituo cha afya Mlandizi katika ziara yake aliyoifanya jana. 
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipata maelezo tembelea kituo cha afya Mlandizi katika ziara yake aliyoifanya jana. 
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea kituo cha afya Mlandizi katika ziara yake aliyoifanya jana. kushoto ni Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi, Dk. Mpola Tamambele, ambaye amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...