Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ameawaonya baadhi ya Wanasiasa kuacha mara moja tabia ya kuwatetea watu wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama kwa tuhuma za kujihusisha na uhalifu.
Rais Magufuli ametoa onyo hilo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam.
“Kuna mwanasiasa anazungumza kuwa hawa watu wamekaa sana lokapu (mahabusu) waachiwe wakati hawa watu wanahusika na mambo ya ajabu katika nchi.
“Kuna watu wamekufa kule zaidi ya 35, maaskari zaidi ya 15 na wanaohusika ni pamoja na hao lakini mtu anatoka anazungumza kwamba wamekaa mno. Unaweza ukaona ‘by implication’ kwamba huyu lazima anahusika kwa njia moja au nyingine”, alionya Rais.
Amewataka wanasiasa wa namna hiyo kujifunza kunyamaza wakati serikali inafanya kazi yake.
Aidha Rais Magufuli alieleza kusikitishwa na mmoja wa wanasiasa ambaye kimsingi hajawahi kusimama hata siku moja kulaani mauaji ya watu wasio na hatia yanayotokea lakini kwa kutaka sifa za kisiasa alisisimama hadharani kutaka wahalifu waachiwe.
Alisema hivi karibuni jeshi la Polisi lilikamata sare 5000 za jeshi na wanaohisiwa kuhusika ni pamoja na ambao tayari wanashikiliwa na vyombo vya dola lakini bado mtu anaingiza siasa kwa kuwatetea wahalifu.
Rais Magufuli ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini, amelitaka jeshi la Polisi kumhoji kwa kina mwanasiasa yeyote anayetetea wahalifu kwani anaweza kuwa nae anahusika.
“Nataka Polisi mfanye kazi zenu, hawa wanaoropoka waisadie polisi kupeleleza. Msiogope cha sura au mwendo wa mtu awe na mwendo wa spidi au pole pole atayaeleza vizuri atakapo kuwa mle lokapu.
Ameeleza kuwa yeye kama Rais moja ya majukumu yake ni kulinda usalama wa Watanzania na kuusimamia kwa nguvu zote na kwamba maendeleo yaliyopo yanakuja kwa sababu nchi ni slalama.
Amewaomba Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao kutanguliza uzalendo na kutetea maslahi ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...