THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Milioni 20 za Biko zaenda Morogoro, Lohai naye avuta mkwanja wake

DROO ya 22 ya waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku, imefanyika leo jijini Dar es Salaam, huku mkazi wa Morogoro, Elizabeth Damian akifanikiwa kutangazwa mshindi wa Sh Milioni 20 zinazotolewa na bahati nasibu hiyo.

Mwanadada huyo kutoka mkoani Morogoro, alitangazwa mshindi katika droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

Akizungumza katika droo hiyo, Kajala aliwataka Watanzania kuendelea kucheza Biko ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kuvuna mamilioni yanayotolewa na Biko tangu kuanzishwa kwake, huku hadi sasa kwa miezi miwili ya Mei na Juni, zaidi ya Sh Bilioni moja zikienda kwa washindi.

Alisema fursa inayotolewa na Biko ni nzuri kwa uchumi wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba wanacheza Biko mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri ya kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, sambamba dau nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili, kianzio cha kucheza kikiwa Sh 1000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ya Biko ikiwa ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

“Tangu Biko ianze kuchezeshwa Tanzania imekuwa ikitoa nafasi kubwa ya Watanzania kuvuna mamilioni, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi kucheza Biko ili nao waweze kuvuna fedha zinazotolewa Biko kwa zawadi za papo kwa hapo pamoja na zile wiki ambazo ndio kubwa zaidi, nikiamini kuwa endapo mtu anafanikiwa kuzipata, naamini atapiga hatua kubwa kiuchumi,” Alisema Kajala.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Yassin Lohai akipiga picha ya shangwe baada ya kukabidhiwa fedha zake katika tawi la Madaraka la NMB jijini Tanga leo mchana. Lohai alikabidhiwa na Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven hayupo pichani.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wa Tanga, Yassin Lohai baada ya kushinda donge nono la Biko Jumapili iliyopita. Kushoto ni Afisa wa NMB, Tawi la Madaraka, jijini Tanga, akishuhudia makabidhiano hayo kwa mshindi wa Biko mkoani Tanga.
Balozi wa Biko Kajala Masanja, kulia akisalimiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, katika droo ya kumtafuta mshindi wa Milioni 20 wa droo ya 22, ambapo Elizabeth Damian alitangazwa mshindi leo asubuhi.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA