MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewasihi wanafunzi wa kike nchini kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha kukatisha masomo yao.
Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa mfululizo kutoka kiwango kimoja cha taaluma kwenda kingine.
Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 23, 2017) alipozungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Vwawa wilayani Mbozi.
Mke wa Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ziara ya mkoa Songwe, aliwaasa wanafunzi hao kutumia wakati huu kwa kusoma kwa bidii na kujiepusha na vitendo viovu.
“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara kwa ajili ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikatishe masomo yenu.”
Mama Mary aliongeza kwamba “utumieni muda huu vizuri ili msije mkaujutia baadae, kwani wakati ni mali ukipita umepita.”
Alisema ni vizuri wakasoma hadi chuo kikuu na kwamba wasikimbilie kufanya mambo yasiyowahusu kwa sasa kwani mshika mawili moja lazima limponyoke.Mke wa Waziri Mkuu alisema wanafunzi hao wakisoma hadi elimu ya juu watakuwa na uwezo wa kutambua jambo lipi ni jema na lipi ni baya.
“Kilichonifurahisha zaidi ni kwa sababu mimi pia ni mwalimu kwa hiyo inavyoona wanafunzi wako vizuri kama hivi nafurahi sana, hivyo nawaomba msome kwa bidii.”
Serikali imetunga sheria kali dhidi ya watu wanaosababisha watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kuwapa mimba au kuwaoa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JULAI 24, 2017

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majalwa akizungumza na wanafujnzi wa Shule ya Sekondari ya Vwawa iliyop[o Mbozi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na watumishi wa umma, viongozi wa dini na viongozi wa taasisi za binafsi kwenye ukumbi wa shule hiyo Julai 23, 2017 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...