MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma Shafi Mpenda, amekifungia kituo cha kitengo cha utafiti wa sayansi ya tiba asili na tiba mbadala kinachojishughulisha na kupima afya za binadamu na kutibu magonjwa mbalimbali cha The King Solomon of Sanitarium clinik hadi hapo wataalam wa afya watakapojiridhisha uhalali wake.

Mbali na kukifungia kituo hicho,Mpenda amesema atawachukulia hatua kali baadhi ya wataalam wake wa idara ya afya walioshiriki kutoa vibali feki vilivyohalalisha kituo hicho kufanya kazi ambayo imeonekana kama kuwatapeli wananchi.

Kwa mujibu wa Mpenda ni kwamba, kituo hicho kupitia kwa mmiliki wake Selemani Nzaganya kimekuwa kikifanya shughuli zake kinyume na taratibu ambapo hata leseni kutoka kwa baraza la tiba asili kimekwisha muda wake tangu tarehe 1 januari mwaka huu,hata hivyo bado akifanya shughuli zake bila kupata leseni mpya jambo ambalo ni kosa kinyume cha sheria.

Alisema, amelazimika kufunga kituo hicho kwa ajili ya kuokoa maisha ya wansanchi kwani hata mtu aliyekutwa akihudumia wananchi hana taaluma yoyote inayomwezesha kuhudumia wagonjwa jambo linaloonekana ni hatari kwa afya za watu.

Kwa mujibu wa Mpenda hii ni mara ya pili kufunga kituo kama hicho na ni kampeni ya kudumu kwa wale wote wanaofanya shughuli za kuwatapeli wananchi wa Madaba ambapo ametoa onyo kwa watu wengine wenye tama ya kupata fedha kwa njia ya ujanja ujanja kutafuta maeneo mengine ya kufanya shughuli zao.

Hata hivyo kwa mujibu wa majirani ambao hawakutaka kutaja majina yao,wameipongeza serikali kwa uamuzi wa kukifungia kituo hicho kwani wamiliki wake walikuwa wakiwaibia wananchi.

Walisema, kituo hicho kimekuwa sehemu ya tatizo kwa sababu hata wananchi wanaohitajika kupata ushauri na matibabu hospitalini wamekuwa wakifika katika kituo hicho kwa kuamini kwamba watapata suluhu ya matatizo yao kumbe wanazidisha ukubwa wa matizo waliyonayo.

Kwa upande wake mtu aliyekutwa akitoa huduma katika kituo hicho Ezakiel Mwakatumbula alisema, wamekuwa wanatoa huduma za matibabu kwa wa magonjwa mbalimbali hasa magonjwa sugu kwa kutumkia dawa za mimea,chakula na matunda.

Hata hivyo alikanusha kufanya shughuli zao kitapeli na kusisitiza kuwa huduma wanazotoa zimekuwa zikiwasaidia sana wananchi kuokoa maisha yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...