MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Bi. Doris Mollel amezinduwa tawi jipya la duka la kadi la Kampuni ya ‘Plus Events Cards’ Mwenge, Sokoni Jijini Dar es Salaam huku akiwataka wajasiliamali wadogo na wakubwa wauzaji wa bidhaa hizo kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo ili wajipatie kipato. Bi. Mollel ametoa kauli hiyo alipokuwa akizinduwa tawi hilo, linalofunguliwa kusogeza huduma za uuzaji kadi za kisasa jumla na rejareja kwa wananchi eneo hilo.

Pamoja na hayo, Bi. Doris Mollel aliwashauri wananchi kupenda kununua bidhaa halisi na kuachana na bidhaa feki kwani zimekuwa na madhara huku zikilikoseshea taifa mapato. Alisema bidhaa nyingi feki haziingii kwa utaratibu rasmi nchini hivyo licha ya madhara kwa watumiaji zimekuwa zikilikosesha taifa mapato.

“…Nashauri Watanzania wenzangu tupende kununua bidhaa halisi zinazoendana na thamani ya fedha tunazotoa. Uzuri sasa hivi wauzaji wengine wamekuwa wawazi wanakwambia hii ni bei rahisi kwa kuwa ni feki na hii ndio bidhaa halisi…tujenge utamaduni wa kutumia bidhaa bora na halisi kwa manufaa yetu na taifa,” alisisitiza Bi. Doris Mollel.

Aidha aliipongeza kampuni ya Plus Events Cards wauzaji wa kadi na maua ya maharusi kwa kusogeza huduma zake eneo la Mwenge na kutoa fursa kwa wajasiriamali kuwatembelea kwa ajili ya kusambaza bidhaa hizo Dar es Salaam na hata mikoani. Aliongeza kuwa hatua hiyo si tu imesogeza huduma kwa wahitaji bali imetoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata bidhaa za kadi kirahisi na kuzisambaza kwa wahitaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la Kampuni ya Plus Events Cards, Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses na Mkurugenzi Mkuu, Raimond Njuu (kushoto) wakishuhudia.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Plus Events Cards, Raimond Njuu (kushoto) mara baada ya kuzindua tawi jipya la Kampuni ya Plus Events Cards, Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses akishuhudia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses (kushoto) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (kulia) sehemu ya bidhaa zinazouzwa na duka hilo mara baada ya kuzinduliwa. Kampuni ya Plus Events Cards, wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja imezinduwa tawi jipya Mwenge Sokoni jijini Dar es Salaam.
Hapa ikikatwa keki ya pongezi na viongozi wa Kampuni ya Plus Events Cards.
Picha ya pamoja ya wageni waalikwa baada ya uzinduzi
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Plus Events Cards mara baada ya uzinduzi. Wa kwanza kushoto na kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa duka hilo tawi la Mwenge Sokoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...