Na Karama Kenyunko, 
Globu ya jamii.

Mkurugenzi wa kampuni ya Golden Shark Mining Ltd, Cuthbert Kishululi amepandishwa katika kizimbani cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha zaidi ya USD milioni mbili, ambazo ni sawa na zaidi ya bilioni nne.
Kishululi (48) anayeishi Salasala jijini Dar es salam , wamesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Respicious Mwijage wa mahakama hiyo.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Pius Hilla amesema, January 4 mwaka 2013 jijini Dar wa Salaam, mshtakiwa kwa nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka ya uongo ambayo ni cheti cha kumbukumbu kuonyesha kuwa hajawahi kufanya uhalifu ( Non- Criminal Certificate) cha 17 August 2015.
Imedaiwa kuwa, cheti hicho kilikuwa na nia ya kuonyesha kuwa, kimetolewa na Munusco United Nations Organization Stabilization Mission in the Democratic Republic of Congo kwenda kwa M/S Delicore Metals Company Ltd, huku akijua kuwa siyo kweli.
Hilla ameendelea kudai kuwa, kati ya Julai Mosi na Agosti 30 mwaka juzi,mshtakiwa kwa nia ya kudanganya, alijipatia USD 2,405,000, ambazo ni zaidi ya milioni nne, kutoka Holism Group Ltd kwa uongo baada ya kujifanya angewapatia kilo 500 za dhahabu kutoka kwenye kampuni hiyo ya Holism kupitia kampuni yake ya Golden Shark Mining Ltd
Katika shtaka la tatu imdaiwa kuwa, kati ya Julai 22 na Agosti 27 mwaka juzi, mshtakiwa alitakatisha fedha hizo kwa kujihusisha kwenye muamala wa USD 2,405,000 na kuelekeza fedha hizo zipelekwe kwenye account namba 010095361111 iliyopo katika bank ya I and M bank kwa jina la Delicore Metals Kampuni.
Aidha imedaiwa kuwa, mshtakiwa alizitoa fedha hizo huku akijua kuwa ni zao la uhalifu wa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka yote, na amerudishwa rumande kwa kuwa shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, imeahirishwa hadi Julai 14 ambapo upande wa mashtaka unatarajia kuongeza washtakiwa wengine katika kesi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...