Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira Jumatano hii amefanya ziara ya kikazi wilayani Rombo. Aliianza kwa kukutana na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya hiyo na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kabla ya kufika kituo cha uhamiaji kati ya Kenya na Tanzania upande wa Holili. 
 Aliendelea na ziara ndani ya wilaya kupitia eneo la mpaka wa Kenya na Tanzania linalotajwa kama njia ya panya ya kutorosha magendo na mahindi toka Tanzania kwenda Kenya. Ziara yake ilifikia kituo kingine cha uhamiaji kati ya Kenya na Tanzania cha Tarakea na kisha kumalizia ziara yake eneo la msitu wa miti ya kupandwa wa Rongai eneo la Kamwanga.
 Ziara ilianza saa tatu asubuhi na kumalizika sa kumi na mbili jioni. Mhe Mkuu wa Mkoa alisisitiza kila Mtumishi kutimiza wajibu wake kwa kuwa na UTU NA UZALENDO. "...Lazima tumpime mtumishi kwa kila siku amefanya kazi gani katika ofisi yake - tangu mlinzi, mfagizi hadi afisa wa juu. Ni lazima tuwajibike. Watumishi lazima mtambue nafasi zenu, mziheshimu na kujua kuwa kazi na nafasi yako ni kiungo cha nafasi na kazi ya mwenzako..."alisema Mhe. Mghwira.
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akilakiwa na watumishi akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Rombo 
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiongea na watumishi alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo.
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akioneshwa maeneo na Katibu Tawala Bw. Abubakar Asenga wakati wa  ziara ya kikazi wilayani Rombo
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akitembezwa maeneo mbalimbali katika  ziara ya kikazi wilayani Rombo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...