MKUU wa Wilaya Kibaha, mkoani Pwani, Mheshimiwa Asumpter Mshama, amewapongeza washindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ na kuwataka kuweka umakini na malengo katika fedha zao wanazokabidhiwa ili wanufaike kiuchumi.

DC Asumpter ameyasema hayo jana katika tawi la NMB, Mlandizi, Wilayani Kibaha, mkoani Pwani katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 zilizokabidhiwa kwa Mshindi wa droo ya 19, Elisiana Simon Laizer, mjasiriamali wa kutengeneza sabuni, mwenye maskani yake Mlandizi, aliyeibuka kidedea katika droo ya 19 ya bahati nasibu hiyo ya aina yake inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu za mikononi za Tigo, Vodacom na Airtel.

Akizungumzia bahati nasibu hiyo ya Biko, DC Mshama alisema michezo ya kubahatisha ina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wao na uchumi wa Taifa kwa kuhakikisha kwamba wanafanya shughuli zenye kuleta maendeleo badala ya kuzitumia kwa mambo yasiyokuwa na msingi.

“Nimeshuhudia kwa macho yangu umekabidhiwa fedha hizi Sh Milioni 20 kutoka kwa watu wa Biko, hivyo nitaanza kukufuatilia hatua kwa hatua ukizingatia kuwa upo katika wilaya yangu na mimi kama DC nimekuja hapa kushirikiana na wananchi ili tupige hatua kiuchumi,” Alisema DC Mshama.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha zake, Elisiana Laizer alisema mbali na kuwa ni mjasiriamali wa kuuza sabuni, lakini hatakuwa na papara katika matumizi ya fedha zake alizokabidhiwa baada ya kushinda Biko droo ya 19, huku akiwa ni mchezaji mzuri wa mchezo huo.

“Nashukuru kwa kupewa fedha hizi lakini kwakuwa ni nyingi sana, nitatuliza akili yangu badala ya kufanya papara katika kuzitumia, maana ndoto yangu ni kuhakikisha kuwa fedha zinakuza uchumi wangu, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu tucheze Biko ili tuweze kuibuka na ushindi wa droo kubwa ya Sh Milioni 20 ya Jumatano na Jumapili,” Alisema.
Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko, Goodhope Heaven kushoto akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Asumpter Mshama katikati wakati wa kumkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 19 ya Biko, Elisiana Laizer kulia mwenye gauni jekundu ndani ya benki ya NMB, Tawi la Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Asumpter Mshama kulia akimkabidhi jumlaa ya Sh Milioni 20, mshindi wa Biko droo ya 19, mjasiriamali wa kutengeneza sabuni, Elisiana Laizer, mwenye maskani yake Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Mheshimiwa Asumpter Mshama wa pili kutoka kulia, akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa Biko wa Sh Milioni 20 aliyepatikana katika droo ya 19, mkazi wa Mlandizi, Elisiana Laizer kulia kwake mwenye gauni jekundu. Kushoto ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven na mmoja wa watendaji wa juu wa benki ya NMB kwenye tawi la Mlandizi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...