KATIBU Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Geofrey Mngereza amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Wasanii litakalofanyika Ijumaa jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib alisema Mngereza atashuhudia michezo mbalimbali itakayofanywa na wasanii na wanamichezo.

Alisema tamasha hilo ambalo awali lilikuwa lifanyike kijiji cha Wasanii Mkuranga limehamishiwa jijini Dar es Salaam sababu kubwa ya kuhamisha tamasha hilo ni kutokana na mvua ya msimu uliopita kuharibu barabara ya kwenda kijijini.

Taalib alisema tamasha hilo sasa litafanyika kwa siku mbili kuanzia Ijumaa Julai 14.7.2017 na kuhitimishwa Jumamosi Julai 15 mwaka huu katika viwanja vya Chuo cha Uhazili, splendid Ilala Bungoni.Alisema mpaka sasa wanatarajia kupokea wanamichezo kutoka sehemu mbalimbali kama vile Mkuranga, Kibiti, Zanzibar na Morogoro ambako zaidi ya wanamichezo 600 wamethibitisha kushiriki.

Baadhi ya michezo ambayo itafanyika ni sarakasi, Tae kwon-do, muziki wa dansi, ngumi, soka,rede,muziki wa asili,wu shuu,ngoma,singeli na michezo mingine.Alisema kampuni ya SBC wanaotengeneza soda za Pepsi imekubali kuwa wadhamini wakuu wa tamasha hilo na kuongeza kuwa milango iko wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza.

Akizungumzia ujenzi wa nyumba zao kijijini alisema mgawo na makabidhiano ya nyumba 14 ndogo,kubwa tatu na viwanja 35 vilivyopimwa utafanyika Julai 16 siku moja baada ya kumalizika tamasha hilo.

Alisema kuanzia sasa wanachama wanaotaka kujenga nyumba zao wenyewe wawasiliane na Shiwata ili wapewe maelekezo na utaratibu wa kufanya usafi kwenye makazi yao.Mwenyekiti alisema utaratibu wa kulipia umeme kupitia mpango wa umeme vijiijini (REA)unaendelea na mikakati ya kukarabati barabara ya kufika kijijini unafanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...