THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Mshabiki wa Man U avamia uwanja kumkubatia Wayne Rooney wakati Everton ikiifunga Gor Mahia 2-1


Mshabiki wa Manchester United aliyevamia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kwenda kumkumbatia Wayne Rooney wakati Everton ya Uingereza  ikichuana na Gor Mahia ya Kenya. Uwanja mzima ulishangilia.
Mpira umekwisha kwa Everton kushinda bao 2-1, magoli yakifungwa na Rooney dakika ya 35 kabla  Tuyisenge wa Gor Mahia kusawazisha dakika mbili baadaye. Goli la ushindi la Everton limepatikana dakika ya 82 kupitia kwa mshambuliaji Kieran Dowell. 

Askari polisi wakimdaka mshabiki wa Manchester United aliyevamia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kwenda kumkumbatia Wayne Rooney wakati Everton ya Uingereza  ikichuana na Gor Mahia ya Kenya - ikiwa ni baada ya kuandika katika Instagram ujumbe unaosadikiwa kuwa wake kwamba atafanya tendo hilo. 

Mshabiki huyo akisindikizwa na polisi.