Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi leo muda mfupi kabla ya kuanza kwa sherehe kutimiza miaka 25 kama kiongozi wa Kiroho katika kanisa la Katoliki jimbo Kuu la Dar es salaam katika kanisa la St. Joseph.
Muadhama Polycarp Kardinali Pengo ni kardinali wa pili kutoka Tanzania, akiwa kateuliwa mara baada ya kifo cha Muadhama Laurean Rugambwa, aliyekuwa kardinali wa kwanza kutoka kusini kwa Sahara. 
Alizaliwa kijiji cha Mwazye, mkoani wa Rukwa, tarehe 5 Agosti 1944. Baada ya masomo ya ngazi mbalimbali, alipewa upadrisho mwaka 1971 na askofu Charles Msakila wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga, akasoma teolojia ya maadili huko Roma, Italia, akijitwalia digrii ya udaktari mwaka 1977. Kisha kufundisha somo hilo kwa muda mfupi kwenye seminari kuu ya Kipalapala (mkoa wa Tabora), baadaye 
alichaguliwa kuwa gombera wa seminari kuu ya Segerea hadi mwaka 1983. 
Aliteuliwa askofu wa Nachingwea tarehe 11 Novemba 1983, akapewa daraja takatifu hiyo na Papa Yohane Paulo II tarehe 6 Januari 1984. 
Tarehe 17 Oktoba 1986 alihamishiwa jimbo jipya la Tunduru-Masasi. Tarehe 22 Januari 1990 alifanywa askofu mwandamizi wa Dar-es-Salaam na mwaka 1992, ambapo Kardinali Laurean Rugambwa alipojiuzulu, akawa askofu mkuu.
Muadhama Polycarp Kardinali Pengo  aliteuliwa na Papa Yohane Paulo II kuwa kardinali tarehe 21 Februari 1998, akikabidhiwa parokia ya Nostra Signora de La Salette mjini Roma. 
Pamoja na majukumu mbalimbali katika idara za Papa, tangu mwaka 2007 hadi 2013 alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika na Madagaska.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...