THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA "WEKA AKIBA NA USHINDE"


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WATEJA wanne wa Mwalimu Commercial Bank PLC wamejishindia zawadi za IPAD na vocha za manunuzi baada ya kuibuka washindi kwenye Droo iliyochezeshwa na benki hiyo kufuatia kweney promosheni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 18, 2017 wakati wa kukabidhi zawadi za washindi, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, (pichani juu), alisema, Droo hiyo ilikuwa wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na benki kwa kufungua akaunti kwa kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.

Akifafanua zaidi Bw. Lutenganya alisema, kampeni hiyo ilizinduliwa Mei 18, 2017 na wamepokea wateja wengi ambao walishiriki kwenye Droo hiyo iliyochezeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha, (Gaming Board of Tanzania).

Aliwaja washindi hao kuwa ni pamoja na Bw. Shukuru Sanga, kutoka Waning’ombe mkoani Njombe ambaye alijinyakulia IPAD, wakati Bw. Benester Lazaro, na Grace Machemba kutoka Dar es Salaam, walijinyakulia vocha za manunuzi kama ilivyo kwa Bi. Joyce Sangusangu kutoka mkoani Dodoma.
Meneja wa Tawi la Samora la Benki ya Mwalimu, (Mwalimu Commercial Bank, Plc), Leticia Ndongole, (kushoto), akimkabidhi IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya “Weka akiba na ushinde” inayoendeshwa na benki hiyo.Hafla hiyo imefanyika leo Julai 18, 2017 kwenye tawi lam benki hiyo Mtaa wa Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam. Wengine ni washindi kutoka kulia, ni Bw. Benester Lazaro na Bi. Grace Machemba wote kutoka Dar es Salaam.
Bw. Lutenganya akiwa na maafisa wa benki hiyo wakati akizungumzia zawadi hizo
Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niaba ya washindi wenzake.