Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe. George  Masaju ametoa wito  kwa Asasi zisizo za kiserikali ( NGO)    kushirikiana na kufanya kazi kwa  karibu na Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu wa Serikali    ili  kupitia ushirikiano huo kukomesha   na hatimaye kumaliza kabisa  changamoto zinazowakabili  watanzania wenye albinism.
Mwanasheria Mkuu ametoa  wito huo  leo  ( Jumatano)wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi  Ikponwosa Ero,  Mtaalamu Huru wa Baraza la  Haki za Binadamu  la Umoja wa Mataifa kuhusu  watu wenye albinism
“  Ningependa  kutoa shukrani zako kwa kuamua kuja Tanzania  na kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali,  hii ni fursa  muhimu kwako    ya kupata taarifa sahihi na rasmi kuhusu  jitihada , juhudi na mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali na taasisi zake katika kukabili  vitendo vya jinai dhidi ya watanzania wenzetu wenye  albinism” akasema Mhe. Mwanasheria Mkuu
Na Kuongeza “ kupitia kwako nikuombe basi  uwahimize   viongozi wa asasi zisizo za kiserikali hususani zile zinazojihusisha na  watanzania wenye  albinism kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na  Ofisi yangu  na Taasisi nyingine za serikali kwa sababu wote tuna nia na lengo moja la  kuwasaidia  watanzania wenzetu”..
Akasema  Serikali  inachukulia kwa uzito wa hali ya juu  makosa  ya kijinai dhidi ya watu wenye albinism na kwamba, watuhumiwa wote ambao wamepatikana na hatia wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria na  sheria kuchukua mkondo wake.
Akasisitiza kwamba  Katiba ya  Jamhuri ya Muungano  imesisitiza sana juu ya haki ya mtu kuishi na kwamba haki hiyo ni kwa watanzania wote bila ya kubagua   wakiwamo  watu wenye  albinism au ulemavu wa aina yoyote.
“ Haki ya mtu kuishi imefafanuliwa na kuelezwa kwa kina kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na haki hiyo  haimbagui mtu mwenye albinisim au  mtanzania yoyote ile na ndio maana  makosa ya jinai  dhidi ya  haki ya mtu kuishi  awaye yeyote yule  yanachukuliwa kwa uzito ule ule”.
 Mwanasheria Mkuu wa  Serikali  Mhe. George Masaju akifafanua    kuhusu namna Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Divisheni ya Mashtaka inavyoshughulikia kwa  kupeleleza na kuendesha kesi za jinai dhidi ya watu wenye albnism. katika maelezo yake  Mwanasheria Mkuu amesema  Serikali inachukulia kwa uzito wa hali ya kipekee matatizo yanayowakabili watanzania wenye ualbino na kwamba juhudi hizo  zimesaidia sana katika kupunguza kwa  kiasi kikubwa matukio ya jinadi dhidi ya   watanzania hao ingawa bado kunachangamoto. 
Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akimsikiliza  Bi. Ikponwosa Ero, Mataalam Huru wa Baraza la Haki za Binadamu  la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye albnism. Mhe. Mwanasheria Mkuu na Bi. Ero walikutana leo  Jijini  Dar es Salaam, ambapo walibadishana mawazo  kuhusu  namna  Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu   inavyoshughulikia matukio ya kijinai dhidi ya watanzania wenye albnism.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...