NA K-VIS BLOG, DODOMA

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani Jafo amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS) na kuhimiza na kjtoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati kama sheria inavyowataka ili kuepuka usumbufu kwa wanachama wakati wa kupata Mafao yao wanapostaafu. 

Mhe. Jafo aliyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa mkoani Dodoma Julai 14, 2017.Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wastaafu hao watajiwa ili kuweza kufanya shughuli za ujasiriamali wakati muda wao wa utumishi wa umma utakapokoma.

Mhe. Jafo amewanyooshe kidole waajiri wenye tabia ya kutopeleka michango ya wanachama katika mifuko yao kitendo ambacho kinasababisha kero kubwa pindi watumishi hao wanapostaafu na kuanza kuhangaikia Mafao yao kutokana na taarifa za uwasilishaji michango katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutokamilika.

“Nitoe rai kwa ndugu zangu watumishi wa umma ambao katika kipindi cha miaka miwili ijayo mtaondoka kwenye utumishi wa umma, yatumieni vema mafunzo haya ili mtakapopata mafao yenu basi tayari mtakuwa na nyenzo ya kuwasaidia kutumia vema fedha mtakazopata kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo, lakini pia kilimo na ufugaji wa kisasa na hatimaye kuyafanya maisha yenu kuwa bora baada ya utumishi wa umma.” Aiasa Mhe. Jafo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akikabidhiwa fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Mfkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, (kulia), baada ya kufungua semina ya Mafunzo kwa wastaafu watarajiwa mkoni Dodoma Julai 14, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akitoa hotuba yake. "Mfuko umetenga kiasi cha shilingui Bilioni 1.3 kwa ajili ya kulipa mafao watumishi 9,552 wanaotarajiwa kustaafu kati ya mwaka huu wa 2017/2018."
Naibu Waziri Jafo akitoa hotuba yake.
Washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...