Na Hamza Temba - WMU - Muheza, Tanga
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kukutana na wakulima 879 wa vijiji vitano katika Tarafa ya Amani Wilayani humo kwa ajili kufanya uhakiki wa malipo ya fidia ya mazao waliyolipwa na Serikali ili kupisha eneo la hifadhi ya msitu wa Derema.
Mhandisi Makani ametoa agizo hilo  katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Msasa IBC, Tarafa ya Amani, Wilayani Muheza kufuatia malalamiko ya wananchi hao kupunjwa malipo yao wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 15 baina Serikali na wananchi wa vijiji hivyo vya Kisiwani, Kwemdim, Msasa IBC, Antakae na Kambi.
Akisoma risala ya wakulima hao mbele ya Naibu Waziri Makani, Mwenyekiti wa Kamati ya wakulima hao, Mohammed Rama Shesha alidai kuwa jumla ya wakulima 1,128 wa vijiji hivyo wanailalamikia Serikali kwa kuwalipa viwango pungufu vya malipo ya fidia ya mazao yao tofauti na viwango vilivyolipwa na Serikali mwaka 2002 kupitia mradi wa FINIDA. Aidha, alidai kuwa kuna baadhi ya mazao pia hayakulipiwa kabisa fidia hizo.
Akizungumzia viwango vya fidia hizo Shesha alisema wananchi walilipwa Shilingi 28,800 kwa mche mmoja wa iliki na Shilingi 11,000 kwa mche mmoja wa mgomba. Alidai viwango hivyo vilibadilika kuanzia mwaka 2005 ambapo walilipwa Shilingi 3,315 kwa kila mche mmoja badala ya Shilingi 5,100 kama ilivyoainishwa kwenye viwango vya Serikali hivyo akaomba walipwe kiasi kilichobakia cha shilingi 1,785.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msasa IBC wilaya ya Muheza mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi ya msitu wa Derema. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaisha Tumbo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati), akimuonesha mwenyekiti wa kamati ya wakulima wa vijiji vitano vya tarafa ya Amani, Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mohammed Ramadhani Shesha viwango halali vya serikali vya kulipia fidia za mazao kwa wananchi waliondolewa katika eneo la hifadhi ya msitu wa Derema wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana kwa ajili ya kutatua migogoro wa hifadhi hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaisha Tumbo.  
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msasa IBC wilaya ya Muheza mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi ya msitu wa Derema.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani, (wa tatu kushoto), akiangalia eneo la Msitu wa hifadhi ya Derema na viongozi wa wilaya ya Muheza Muheza wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo jana kwa ajili ya kutatua mgogoro wa hifadhi hiyo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...