Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mjini Kahama, Shinyanga jana. Klabu hiyo imeanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Katikati ni mmoja wa wateja, Salum Selemani na Joshua John (kulia), Ofisa Masoko wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kutoka ofisi ya Mwanza.
 Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa mjini Kahama, katika semina iliyoandaliwa kabla ya  uzinduzi  rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC hiyo iliyoanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Hafla ya uzinduzi ilifanyika mjiini Kahama, Shinyanga jana.
 Meneja wa Kanda wa NBC, Daudi Mfalla (kulia), akizungumza wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi  rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC  iliyoanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara wadogo na wakati wa NBC, Evance Luhimbo.
 Baadhi ya wateja wa NBC mjini Kahama waliohudhuria uzinduzi wa B-Club ya benki hiyo, wakijipiga picha ‘selfie’ pamoja na bango lenye picha inayoonyesha kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni baadhi ya shamrashara zilizopamba uzinduzi huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...