Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwa wanawaandaa watu kupiga picha katika eneo la Nje mara baada ya watu kujaa ndani na kulazimika  kuongeza mashine ndani ya maonesho ya Sabasaba ambapo hitaji la watu kupata vitambulisho vya Taifa limekuwa kubwa
 Msululu wa watu wakiwa katika eneo la nje ya banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakisubiri kupatiwa huduma kwa ajili ya kupata vitambulisho ndani ya Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Hifadhi  hati  kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa 'NIDA'  Bi. Rose Mdami  akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam aliyefika kupata huduma ya Kitambulisho cha Taifa katika banda lao lililopo  katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba
Foleni ya kupata vitambulisho katika banda la ndani la NIDA ikiwa imeshika kasi kuliko kawaida hali iliyowalazimu kuongeza vifaa na watumishi wa kufanyakazi katika Viwanja vya Sabasaba
Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Bw. Said Said akiwa amezungukwa na wananchi waliofika kupata vitambulisho vya Taifa katika viwanja vya Maonesho Sabasaba katika eneo la nje na kuwapa maelzo namna ya kupata Vitambulisho vya Taifa
Sehemu ya wananchi wakiwa wamekaa chini wakisubiri foleni yao ifike ili waweze kuchukua Vitambulisho vya Taifa kutoka NIDA
Maofisa  kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) wakiwa Wamezungukwa na wananchi waliofika kupata vitambulisho vya Taifa. katika viwanja vya Maonesho Sabasaba.
Picha na Humphrey Shayo, Gobu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...