Mamlaka ya Vitambusho vya Taifa (NIDA) imekuwa moja ya Taasisi zilizofanya vizuri katika maonyesho ya Sabasaba mwaka huu kwa kupata tuzo ya Banda Bora katika kundi la Wizara za Serikali na Taasisi “Best Exhibitor Government Ministries & Agencies” kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 41 Sabasaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Dar-es-salaam. 
Takribani kampuni za Ndani 2500 zikiwemo Wizara na Taasisi za Serikali zinashiriki maonyesho hayo, pamoja na kampuni za kigeni 500 zinazowakilisha Nchi 30 duniani.
Maonyesho hayo yaliyoanza Tarehe 28 June 2017 yanatazamiwa kumalizika Julai 13, 2017. Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) katika maonyesho ya mwaka huu imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwa wananchi zinazohusu Utambuzi na Usajili wa Watu  ikiwemo huduma ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa na uchukuaji alama za Kibailojia, kusaidia wananchi waliokwisha sajiliwa na hawajapata vitambulisho vyao, kujua hatua za Maombi yao pamoja na kutoa Elimu kwa umma kuhusu faida, umuhimu na matumizi mapana ya Kitambusho cha Taifa katika ukuzaji Biashara na maendeleo ya Viwanda sambamba na kauli mbiu ya Maonyesho hayo “Ukuzaji wa Biashara kwa maendeleo ya Viwanda.
NIDA imehakikisha ushiriki wao katika Maadhimisho ya mwaka huu unaendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu” kwa kuhakikisha wananchi wanaosajiliwa katika siku 13 za maonyesho hayo wanapata Vitambulisho vyao ndani ya siku hizo.
  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Alphonce Malibiche akipokea tuzo toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni. NIDA ilikuwa mshindi wa kwanza katika kundi la banda bora kwa Wizara na Taasisi za Serikali.


  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Alphonce Malibiche akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE  Mhe. Christopher Chizza baada ya kupokea tuzo toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni. NIDA ilikuwa mshindi wa kwanza katika kundi la banda bora kwa Wizara na Taasisi za Serikali.

Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Alphonce Malibiche akipongezwa na wakuu wa vyombo vya ulinzio na usalama baada ya kupokea tuzo toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni. NIDA ilikuwa mshindi wa kwanza katika kundi la banda bora kwa Wizara na Taasisi za Serikali.


 Baadhi ya Watumishi wa NIDA walioshiriki kufanikisha Maonyesho hayo wakiwa na nyuso za furaha baada ya kupokea Tuzo ya ushindi. Kutoka kulia ni Edna Wanna, akifuatiwa na Agnes Gerrald, Raymondn Sengate na Sarah Mashalla.
 Katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na mratibu wa Banda la Maonyesho la NIDA akiwa ameshikilia Tuzo ya Ushindi pamoja na Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho (kushoto) na kulia ni Ndugu Jamal Kaoneka wa Idara ya Uhamiaji wadau wakuu wa NIDA katika kufanikisha Usajili wa Vitambulisho.
Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa TRL ndugu Masanja Kadogosa akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa wa NIDA baada ya kutembelea Banda la NIDA na kuwapongeza kwa ushindi wa kishindo. Wengine katika picha kushoto ni ndugu Gideon Ndalu Mkurugenzi wa Mifumo ya Tehama NIDA na katikati ni Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...