Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais
Bwana Richard Muyungi (kushoto)
akikabidhi kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na
zisizoharibu tabaka la ozoni
(Refrigerant Identifier) kwa Mkufunzi wa
Chuo cha Ufundi stadi (VETA) Bwana Daudi Kadinda wakati wa makabidhiano Ofisini
kwa Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais
Bwana Richard Muyungi (kushoto) akikabidhi kifaa kinachotumika kutambua gesi
zinazoharibu na zisizo haribu tabaka la ozoni(Refrigerant Identifier ) kwa
Afisa toka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bwana Arnold Mato, wakati wa
makabidhiano Ofisini kwa Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais
Bwana Richard Muyungi akipeana mkono na Wataalamu kutoka Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) na Chuo cha ufundi Stadi
VETA-Chang'ombe mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya vinavyotumika kutambua gesi
zinazoharibu na zisizoharibu tabaka la
ozoni.
Pichani kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na
zisizo haribu tabaka la ozoni(Refrigerant Identifier ) kinavyoonekana kwa
ndani.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya
Makamu wa Rais Bibi Magdalena Mtenga
akijadiliana jambo na Wawakilishi toka TBS na VETA-Chang'ombe mara baada ya
makabidhiano hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...