THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Phillip Luberege wa Dar es Salaam azoa Sh Milioni 20 za Biko

FUNDI ujenzi Phillip Luberege mwenye maskani yake Gongolamboto jijini Dar es Salaam, ametangazwa kuwa mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, akipatikana katika droo ya 20 ya kuwania Sh Milioni 20.

Luberege ametangazwa mshindi leo jijini Dar es Salaam katika droo ya 20 iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, akishirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mshindi huyo amepatikana baada ya kupatikana kwa washindi wa mikoani kiasi cha kuashiria kwamba kumekuwa na mwamko mkubwa kutoka kona zote za Tanzania kuchangamkia mchezo wao kwa watu kuchangamkia fursa ya ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

Alisema kwamba mchezo wao wa Biko ni rahisi kucheza pamoja na kushinda, kwa sababu unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni yao ni 505050 na kumbukumbu yao ni 2456, huku kiasi cha kuanzia kucheza kikiwa ni Sh 1000 na kuendelea.

“Sh 1000 ya kucheza Biko inampa mshiriki wetu nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambapo hufanyika Jumatano na Jumapili, huku mpaka sasa Biko ikitoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi miwili ya Mei na Juni pekee,” Alisema.

Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 aliyopata mkazi wa Gongolamboto, Phillip Luberege. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
Kajala Masanja kulia akiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.