THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

RAIS DKT MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU YA KIKAZI MKOANI KIGOMA.

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

RAIS Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kuanza ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine atazindua barabara zenye kiwango cha lami na mradi wa maji.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa Rais atawasili mkoani Kigoma kupitia Wilaya ya Kakonko tarehe July 21 akitokea Mkoani Kagera ambapo atafanya uzinduzi wa barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutokea Nyakanazi hadi Kibondo yenye kilometa 50.

Mkuu wa Mkoa alisema pia siku hiyo Rais atafanya mkutano wa hadhara na wananchi katika Wilaya ya Kakonko ili kusikiliza kero zao mbali mbali,pia Rais ataelekea Wilayani Kasulu ambapo pia atazindua barabara kidahwe mpaka kasulu iliyojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63.

Maganga alisema July 22 Rais ataweka jiwe la msingi mradi wa maji uliopo Manispaa ya Kigoma Ujiji na kisha atafanya mkutano wa hadhara na wananchi katika uwanja wa Lake Tanganyika.

Na July 23 Rais ataelekea Wilayani Uvinza kwaajili ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji uliopo katika Kata ya Nguruka eneo la amani na baadae mkutano wa hadhara na wananchi.

Maganga amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais kwani hii ni ziara yake ya kwanza tokea uchaguzi Mkuu ufanyike.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara ya Rais Dkt John Pombe Magufuli Mkoani Kigoma.