Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamini William Mkapa amewasili wilayani Chato mkoani Geita ambapo leo Jumatatu Julai 10, 2017 atakakabidhi nyumba kumi kwa hospitali ya wilaya ya Chato zilizojengwa kwa ufadhili wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Mkapa Foundation, anayoiongoza. 
 Mhe. Mkapa ambaye ameambatana na Mkewe Mama Anna Mkapa wamepokelewa na wenyeji wao ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli. Katika Msafara huo pia Rais mstaafu Mkapa ameambatana na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharn Yoshida ambaye siku hii atakabidhi mashine ya kukamulia mafuta ya Alizeti kwa chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato – AMCOSS. 
Rais Mstaafu Mhe Benjamini William Mkapa anatarajiwa pia kuhudhuria mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na Mwenyeji wake Rais Magufuli utakaofanyika katika uwanja wa Mazaina ulioko mjini Chato majira ya saa tatu asubuhi hii kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita. Kushoto ni Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita. Balozi huyo wa Japan katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi mtambo wa kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine) uliojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa nyumbani kwake Chato mkoani Geita
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa pamoja na wageni mbalimbali waliofika Chato kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotarajiwa kufanyika kesho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita Josheph Kasheku Msukuma aliyefika Chato pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita. 
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...