Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Tanzania Mhe. Ally Hassan Mwinyi (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri (wa tatu kushoto) juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel jana jijini Dar es salaam baada ya kiongozi huyo kutembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Tanzania Mhe. Ally Hassan Mwinyi (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri (wa pili kushoto) juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel jana jijini Dar es salaam baada ya kiongozi huyo kutembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara nchini Christopher Chiza (wa pili kulia).
Msanifu Maabara kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Sebastian Magulu (kushoto) akizungumza wakati wa kumtoa damu Mkazi wa Mbagala, Husna Hamisi (katikati) katika banda la Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel alipotembelea banda hilo jana jijini Dar es salaam ili kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo. Zantel kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu Salama wameandaa utaratibu wa uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo katika kipindi hiki cha maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Kulia ni Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa.
Mkazi wa mkoa wa Morogoro, Peter Albano akichangia damu katika banda la Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel alipotembelea banda hilo jana jijini Dar es salaam ili kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo. Zantel kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu Salama wameandaa utaratibu wa uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo katika kipindi hiki cha maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Anayetoa damu ni Msanifu Maabara kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Sebastian Magulu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...