RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amerejea nchini leo akitokea nchini Uingereza. 
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali pamoja na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walimpokea Dk. Shein wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
 Dk. Shein katika safari hiyo maalum ya nchini Uingereza, alifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Watendaji wengine wa Serikali. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein akiteremka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Uingereza kwa ziara maalumu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Shada la mauwa kutoka kwa Mtoto Naifat Faudhi wakati wa mapokezi yake leo baada ya kuteremka katika Ndege ya Serikali  mara ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akirejea Nchini Uingereza kwa Ziara maalum
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein akisalimiana na Makamo wa Pili wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Idi mara baada ya kuwasili katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Uingereza kwa ziara maalumu

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliofika kumpokea  baada ya kuwasili katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Uingereza kwa ziara maalumu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliofika kumpokea  baada ya kuwasili katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Uingereza kwa ziara maalumu. 
Picha na IKULU na Yussuf Simai - MAELEZO ZANZIBAR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...