THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

RC MAKONDA AGAWA KOMPYUTA KATIKA HALMASHAURI ZA JIJI LA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh.Paul Makonda leo amekabidhi kompyuta za kisasa 50 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 170 kwa Manispaa tano za Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Watu wa Jiji na Mkoa kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi.

Katika mgawanyo huo kila Manispaa imepatiwa kompyuta nane (8) huku Ofisi ya Jiji wakipatiwa kompyuta tano (5) na Ofisi ya Mkoa wakipatiwa kompyuta tano (5) ikiwa ni ufadhili wa kampuni ya ulinzi ya TAMOBA Company Ltd iliyomuunga Mkono RC Makonda kutokana na kuhamasika na utendaji kazi wake mzuri.

Makonda amesema Kompyuta hizo zitawekewa Mfumo wa kisasa ujulikanao kama Dar Ardhi E.System utakaoziunganisha idara zote zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi (One stop Center) ili kurahisisha Mwananchi kupata kibali cha ujenzi ndani ya muda mfupi, ambapo mwananchi atakuwa na uwezo wa kutuma maombi ya kibali cha ujenzi kwa kutumia simu ya mkononi mwake au Computer hata akiwa nyumbani na akapewa majibu yake kwa haraka.

“Kazi yangu kubwa ni kupunguza mateso,malalamiko na kero za Wananchi dhidi ya maswala ya Ardhi, na namna mbili za kupunguza ni pamoja na kuwawezesha watendaji kuwa na nyenzo na vifaa vitakavyorahisisha kufanya kazi zao kisasa zaidi kuendana na kasi ya Rais wetu Dr.John Magufuli, na pili ni kusimamia uwajibikaji kwamba kila mmoja anatekeleza majukumu yake ili Mwananchi wa Mkoa wa Dar es salaam asipate adha na mateso aliyokuwa akiyapata kwenye Sekta ya Ardhi.

Umuhimu wa kutoa vibali vya ujenzi ni jambo lisilopingika hasa katika mji huu unaokuwa kwa kasi barani Afrika” Alisema Makonda. Aidha kompyuta hizo zitawekewa Mfumo maalumu utakao kuwa ukikusanya Maoni na mapendekezo ya wananchi ambapo wananchi watakuwa na fursa ya kutuma maoni yao na kero mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta ya Ardhi.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Mkaonda akipanga kompyuta mara baada ya kupokea kuoka Kampuni ya TAMOBA Company Ltd ya jijini Dar es salaam. 

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiangalia kompyuta mara baada ya kupokea kopmyuta hizo zilizotolewa na Kampuni ya TAMOBA Company Ltd ya jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda (kushoto)akikabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ialala,Msongela Palela Computer za kisasa 50 zenye thamani ya zaidi ya Shilling Million 170 kwa Manispaa tano za Mkoa wa Dar es salaam pamoja leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa ,Paul Makonda akiteta jambo na watendaji wa kampun ya ulinzi ya TAMOBA Company Ltd iliyomuunga Mkono Mheshimiwa Makonda kutokana na kuhamasika na utendaji kazi wake mzuri.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.