Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhiwa gari aina ya Wingle 5 na Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).

Akielezea sababu ya kukabidhi gari hiyo kwa serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Jianguo Liu ameeleza kuwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli.

Meneja Liu ameeleza kuwa gari hiyo inathamani ya shilingi milioni 55, hivyo itumike kutatua changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake RC Makonda amewashukuru wahisani hao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia msaada huo kama ilivyokusudiwa, huku akieleza kuwa utaratibu wa kulitumia gari hilo utatokana na maoni ya wananchi ambapo watapiga kura kupitia namba maalumu na kueleza gari hilo liende kwenye idara ipi, kwa mfano idara ya elimu, afya, polisi nakadhalika, zoezi hilo litachukua siku kumi.

RC Makonda ameongeza kuwa serikali yake itaendelea na utaratibu huo wa kupigia kura magari yaende kwenye idara ipi ili kuchochea ufanisi wa kazi na wanachi ndiyo watakao kuwa waamuzi wa hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhiwa gari na Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akilikagua gari hilo.
Muonekano wa gari hilo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwashukuru wahisani Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).kwa kukabidhi gari leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu kakizungumza machache kabla ya kukabidhi gali hilo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmauel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...