Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la kisasa la huduma za dharura Hospitali ya Temeke ambalo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi Million 800 linalofadhiliwa na ubalozi wa Japan Nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mheshimiwa Makonda amesema jengo hilo litakuwa na uwezo wa kusaidia zaidi ya watu 2,000 kwa siku ambapo litakuwa na chumba cha upasuaji,chumba cha ICU,vyumba vya uangalizi maalumu wa wagonjwa pamoja na vyumba vya madaktari.

Aidha jengo hilo litakuwa na vyumba maalumu vya watoto (njiti) akinamama na wababa ambapo lengo ni kuhakikisha mgonjwa yoyote wa dharura iwe wa ajali,upasuaji kwa kinamama wajawaziito,malaria ya ghafla,moto na wanaobanwa na kifua wanapatiwa huduma ya haraka ambapo kwa hatua hiyo itasaidia kupunguza mlundikano wa wagonjwa wa dharura Hospital ya Taifa Muhimbili kama Rais Dkt.Magufuli anavyotaka.

“Mimi nimeshuhudia watu wengi wakipoteza maisha kwa kukosa huduma za dharura, hii ndio iliyonisukuma kutafuta kila njia ili wananchi wangu wasipoteze maisha kwasababu tu ya kukosa hutuma ya haraka, nikaamua kumtafuta balozi wa Japani na kumshirikisha jambao hili, Balozi aliponisikiliza na kunielewa akakubali kuniunga mkono katika mapambano yangu ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi hasa wanyonge na ameshanipa fedha kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo na hivi tunavyoongea tayari mkandarasi ameanza na ujenzi” Alisema Makonda.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  akikata utepe kwa kushirikia na Mkuu wa Wilaya wa Temeke,Felix Lyaniva pamoja Mwakilishi wa Balozi wa Japani Nchini,Hiroyuki Kubota,kwenye hafla fupi ya uwekeji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la kisasa la huduma za dharura Hospitali ya Temeke, ambalo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi Million 800 linalofadhiliwa na ubalozi wa Japan Nchini Tanzania.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akipongezana na Mwakilishi wa Balozi wa Japani Nchini Tanzania,Hiroyuki Kubota.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda na viongozi wa halmashauri ya manispaa ya temeke wakikagua ujenzi wa jengo la huduma za dharura.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...